Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga amesema atajaribu
kukaa na wasanii wa muziki Diamond na Ali Kiba na kuangalia tofauti zao ili kuwapatanisha
Akizungumza na The Sporah Show hivi karibuni, Kusaga amedai kuwa alikuwa hatambui kama
wasanii hao wana matatizo kwenye kazi zao na kuahidi kuwa ataliangalia tatizo lao.
“Kiukweli wote ni watoto wangu, Diamond ananipa heshima sana mimi ,namshukuru, Ali Kiba
is the same, nafanya nao kazi na sijawahi kugombana nao. Lakini sijui kama walikuwa wana
tatizo ndo nasikia sasa, lakini ngoja nijaribu kuwapigia ni find out kwanini? na kuna tatizo
gani between wao, lakini sijawahi kujua wana matatizo hayo.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni