Jumatatu, 16 Juni 2014

AUNT EZEKIEL: Bado sijaona mwanaume wa kunizalisha


Wakati rafiki yake kipenzi, Wema Sepetu akidaiwa kunasa mimba ya Diamond , Aunt Ezekiel yeye amesema bado hajaona mwanaume anayeweza kumtia mimba na hatimaye kuitwa baba wa watoto wake.


Akipiga stori na mwanahabari wetu , Aunt Ezekiel amedai kuwa kuna wakati unaweza kumuona yupo kwenye ndoa au uchumba lakini haimaanishi kuwa kuwepo katika mazingira hayo ndo anaweza kuzaa au kushika mimba kwani suala hilo kwake ni kubwa sana na hajafikiria kama linaweza kutokea kwa sasa…






“Siyo kwamba sina uwezo wa kubeba mimba, hapana, suala kubwa hapa ni kwamba bado sijaona mwanaume wa kunizalisha.

“Ni kweli nilikuwa kwenye ndoa lakini sikutaka kubeba mimba na ndo maana hadi sasa hivi nipo kama ninavyoonekana,” alisema Aunt Ezekiel.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni