Mwanamke mmoja mkazi wa Kintinku, Wilayani Manyoni mkoani Singida amejikuta akimwaga machozi baada ya kujifungua mtoto mwenye kichwa cha ajabu ( tepe tepe).
Tukio hilo limetokea jana asubuhi katika hospitali ya Kintinku Health Center iliyopo Wilayani Manyoni…..
Akiongea na Mpekuzi kwa sharti la kutotajwa jina lake kwa madai kuwa yeye si msemaji wa hospitali hiyo, Mkunga mmoja wa hospitali hiyo amedai kuwa mama huyo alifikishwa hospitalini hapo akiwa katika hatua za mwisho kujifungua.
“Alifikishwa hapa akiwa katika hatua za mwisho . Hakuwa na kadi yoyote ya Clinic kwa kuwa hakuwahi kuhudhuria Clinic tangu abebe mimba hiyo.
“Pamoja na kutokuwa na kadi ya Clinic, tulianza kumsaidia kujifungua, lakini mtoto aliyezaliwa alikuwa ni wa tofauti kidogo na alikuwa amefariki dunia.Kichwa chake kilikuwa tepetepe na kimebonyea bonyea.
“Ilikuwa ni ngumu kwetu kutambua tatizo alilokuwa nalo mama huyo kwa kuwa hakuwa na kadi yoyote ya Clinic ambayo ingeweza kutusaidia kujua maendeleo ya mtoto huyo alipokuwa tumboni “, alisema Mkunga huyo.
Mpekuzi ilifanya mahojiano na mama huyo ambaye naye alionyesha kushangazwa na tukio hilo na kusema hajui tatizo lililomfanya ajifungue mtoto huyo kwa kuwa hakuwahi kusikia maumivu ya aina yoyote wakati wa ujauzito huo hadi alipofikia hatua ya kujifungua….
Katika mahojiano hayo, mama huyo alisema kuwa huo ni uzao wake wa 6 na hajawahi hudhuria Clinic
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni