Jumapili, 15 Juni 2014

VIDEO: DIAMOND AELEZEA WALICHOZUNGUMZA NA MENEJA WA TREY SONGZ, KEVIN LILES ALIPOKUTANISHWA NAYE NA RAIS KIKWETE MAREKANI


Hivi karibuni Diamond Platnumz alipata nafasi ya kukutana na mtu mkubwa
katika industry ya muziki wa Marekani Kevin Liles, ambaye ni rais wa
zamani wa Def Jam na kwasasa ni meneja wa muimbaji wa R&B Trey Songz
na Big Sean.
Bongo5 ilitua Durban kwaajili ya Tuzo za MTV MAMA zilizofanyika
Jumamosi iliyopita, ilipata nafasi ya kufanya Exclusive Interview na
Diamond kabla ya tuzo hizo, pamoja na mengine Platnumz ameelezea
walichozungumza alipokutanishwa na Liles na Rais Kikwete nchini
Marekani.

“Ilikuwa ni namna ya kuangalia nafanya vipi katika soko la Amerika na
dunia nzima” Alisema

Diamond. “So nilipokutana na Mheshimiwa Rais
akaniambia kitu gani unahitaji nikusaidie, nikamwambia connection, kila
kitu ni connection njia ya kuweza kuingia katika soko la Amerika na
dunia nzima, so akasema basi nitakukutanisha na mtu fulani ambaye
naamini anaweza akakusaidia, so akamtafuta akampigia simu nikaonana
naye(Kevin Liles)”.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni