NCHI za wenzetu staa kupiga picha za
utupu si kitu kigeni lakini Kibongobongo sheria na maadili ya Mtanzania
hayaruhusu kufanya hivyo.
Aunt Lulu.
Licha ya kubanwa na sheria pamoja na
maadili, wapo wasanii ambao kwa nyakati tofauti walijikuta katika adha
ya kupigwa kama si kujipiga picha za utupu kisha zikazagaa mitaani.
Wapo waliotajwa kupiga picha hizo kwa
kusaka umaarufu, waliopigwa na wapenzi wao kisha wakazivujisha lakini
wengine imedaiwa kuwa wamezivujisha wenyewe na kusingizia zimevujishwa
na wapenzi wao.
Ifuatayo ni orodha ya wasanii mbalimbali Bongo ambao waliwahi kukwaa skendo ya picha za utupu:
Wema Sepetu.
Wema Sepetu:
Mwaka 2010 picha yake ya utupu
ilizagaa mtandaoni huku ikidaiwa kuwa chanzo cha kusambaa kwake ni
boifrendi wake ambaye alimpiga na kuzisambaza. Kama hiyo haitoshi, mwaka
huu mrembo huyo alidaiwa kuposti picha zake nyingine za utupu katika
mtandao wa Instagram.
Huyu ni Miss Dar Indian Ocean ambaye
pia ni Miss Kinondoni namba 2 mwaka jana, mrembo huyo hivi karibuni
amejikuta akipata aibu baada ya picha yake ya utupu kuvuja. Ilidaiwa
kuwa alifanya hivyo kwa azma ya kusaka umaarufu.
Jack wa Chuz:
Ni bonge la ‘actress’ Bongo Movie,
mwaka 2012 alipigwa picha za utupu na kusambazwa kila kona ya Jiji la
Dar. Ilidaiwa kuwa kuna mtu alizichukua picha hizo kutoka kwenye simu
yake na kuzisambaza kwenye vyombo vya habari.
Agness Masogange:
Nini picha! Yeye ilivuja video yake
ya utupu kabisa. Ilisambaa kama njugu katika mitandao ya kijamii mwaka
jana. Vyanzo makini vilidai kuwa video hiyo alipigwa na mpenzi wake na
haikujulikana mara moja chanzo kilichozivujisha.
Jacqueline Wolper:
Pamoja na heshima kubwa aliyonayo
kwenye soko la filamu, mapema mwaka huu staa huyo amejikuta akichafuka
baada ya picha yake ya utupu kuanikwa gazetini. Ilidaiwa kuwa picha hiyo
alipigwa kwenye bethidei ya msanii mwenzake.
Marry John:
Msanii wa filamu Bongo, Mary John
‘Maua’ mwaka jana alijipatia jina baada ya kupiga picha kadhaa za utupu
na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii yeye mwenyewe.
Aunt Lulu:
Mara kadhaa amekuwa akitengeneza
vichwa vya habari magazetini kwa kupiga picha za utupu. Mfano hai ni
picha ambazo alipiga mwaka jana, ambapo alidai kuwa alipigwa bichi
alipokwenda ‘kula bata’.
Lulu:
Mwaka 2010 alijikuta akichafuka kwa
kutajwa kwenye skendo ya kupiga picha ya utupu. Alipoulizwa kuhusiana na
picha hiyo alikanusha kuwa si ya kwake na kudai kuwa ilitengenezwa na
watu ili kumchafua.
Jack Patrick:
Kwa upande wake suala la kuvuja kwa
picha zake za utupu siyo ishu. Mwaka jana ilidaiwa kuwa aliziposti picha
zake za utupu kwenye mtandao wa BBM, haileweki ni kwa nini huwa
anafanya hivyo.
Isabela ‘Vai wa Ukweli’:
Huyu ni chipukizi kwenye anga la
filamu Bongo, mara kadhaa amepigwa picha za utupu na kusambazwa kwenye
vyombo vya habari. Imedaiwa kuwa hufanya hivyo kama kutafuta mlango wa
kutokea kwenye ustaa.
Maadili ya Mtanzania yanatukataza
kufanya vitendo vya namna hii hivyo ni vyema wahusika wakawa makini,
waepuke kupiga wala kuhusika kusambaza picha zao za utupu kwa namna
yoyote ile.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni