Ijumaa, 13 Juni 2014

FABREGAS ATUA CHELSEA KWA PAUNI MILIONI 30



KIUNGO wa Barcelona na Hispania, Cesc Fabregas amejiunga na Klabu ya Chelsea kwa pauni milioni 30 kwa mkataba wa miaka mitano. Fabregas atavaa jezi namba nne kama aliyokuwa akivaa Arsenal na Barcelona.
Kiungo huyo ameishukuru Barcelona ambapo amekaa miaka mitatu kwa furaha.
"Ilikuwa timu yangu ya utotoni na nitajivunia kila mara kupata nafasi ya kuchezea timu hiyo kubwa"
"Nahisi bado sijamaliza kazi katika Premier League na kwa sasa ni muda muafaka mimi kurudi England
"Nilifikiria ofa mbalimbali kwa makini na naamini nilifanya uamuzi sahii
Chelsea inaendana na matarajio yangu kwa kiu yao ya kushinda mataji. Wana kikosi cha ajabu na meneja wa hali ya juu". Alisema Fabregas

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni