Jumatano, 18 Juni 2014

AMANDA WA BONGO MOVIE AMCHANA LIVE FLORA MBASHA


MSANII wa kike kutoka tasnia ya filamu Bongo, Tamrina Posh ‘Amanda’ amemfungukia mwimbaji wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha akimshauri kuacha kumwanika mumewe, Emmanuel Mbasha kwenye vyombo vya habari.

Msanii wa kike kutoka tasnia ya filamu Bongo, Tamrina Posh ‘Amanda’. Flora na mumewe Mbasha, wapo kwenye mgogoro wa kifamilia huku mwanaume akikabiliwa na tuhuma za ubakaji, sakata ambalo limekuwa likiripotiwa sana katika kipindi hiki, huku kila mmoja akimtuhumu mwenzake mambo mbalimbali.


Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Amanda alisema kitendo cha Flora kuendelea kuanika mambo ya mwenzi wake hakina maana, akifafanua kuwa siri za ndani ya nyumba zinapaswa kuhifadhiwa.
“Vyovyote inavyokuwa, lakini inatakiwa Flora atambue kuwa, Mbasha (Emmanuel) ni mumewe.



Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha. Hata kama amemkosea kwa kiasi gani, bado walikuwa na nafasi ya kuyazungumza hayo mambo nyumbani kama familia na siyo kuyaanika kwenye vyombo vya habari,” alisema Amanda na kuongeza:

“Nasisitiza haya ni mambo ya kifamilia, walitakiwa kwenda kwa wazazi, ndugu waliowazidi umri au kwa viongozi wa dini, yangezungumzwa na yangeisha tu badala ya kuwa hivi yanavyoendelea. Yeye ni kioo cha jamii, tena mtumishi wa Mungu, aangalie mara mbili.” Share :

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni