Wameshatembea nchi nyingi duniani ikiwemo mara 2 walizokuja Tanzania pekee ndani ya miaka 10 iliyopita
PETER na PAUL OKOYE ni mtu na kakaye ambao wana historia ya kipekee sana kwenye Muziki wa Afrika na hawaishi kueleza mahali Mungu amewatoa na walipo sasa
Wametamba na vibao vyao motomoto kama ROLL IT,IFUNANYA,TEMPTATION,na sasa wanatamba na vibao kama ALINGO,PERSONALLY na TESTIMONY ambavyo vinaendelea kuwaweka juu kwenye ramani ya Muziki duniani
Wimbo huu wa TESTIMONY unaaminika kubeba maana kubwa na Ushuhuda wa Maisha yao wao wawili,kabla hawajawa hapo walipo leo,wakiwa na uwezo wa kuishi popote,kwenda popote,na kununua chochote wapendacho
Wiki hii,PETER ametambulisha Magari yake mawili,BENTLEY GT na WRANGLER JEEP,yote yakiwa ni ya Mwaka 2014
Magari haya,miaka michache iliyopita wangekuwa wakiyatamani tu kwenye TV wakiona wanamuziki wakubwa duniani kama AKON,LIL WAYNE,DRAKE,na 50 CENT wakiyaendesha,lakini leo hii na wao wanao uwezo wa kuyamiliki
ANGALIA UTAJIRI WAO HAPA CHINI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni