Unaambiwa Dunia haina siri, sasa ile
siri waliokua wakiiweka kati wanamuziki Diamond Platnumz, Ommy Dimpoz
pamoja Victoria Kimani basi imeshajulikana....
UTANGULIZI
Unajua ilikua iwe suprise kwa mashabiki
yani Video itoke alafu ijulikane walikua wameenda Uingereza kufanya
shooting sasa katika pita pita ya mtandao huu wa Blog ya Vijana umekuta
picha iliowekwa wenye akauti ya Babu Tale ambae nae yupo Uingereza.
Tukumbuke kwamba kulikua na kawivu flani
ndani ya moyo wa Wema Sepetu ambae ni mchumba wa Diamond Platnumz, ni
baada ya stori kuenea kwamba Diamond alitoka kimapenzi na Msanii wa
Kenya Victoria Kimani kipindi kile walipoenda kufanya nyimbo ya Cocoa na
chocolate iliofanyika nchini South Afrika iliofanywa na wasanii tofauti
kutoka Afrika. Baadae Victoria kimani alitua nchini Tanzania kiufanya
nyimbo ya Prokoto aliomshirikisha Diamond Platnumz na Ommy Dimpoz,...
nyimbo imetoka hata wiki haijamaliza.....
UKWELI NI UPI SASA
Diamond na iyaya wanashoot video ya nyimbo mpya ya Diamond aliomshirikisha Iyaya ushahidi kupitia Video Director wao
Diamond Platnumz pamoja na Ommy Dimpoz wameenda kushoot video ya Prokoto waliofanya na Victoria Kimani,
Haya bibie Wema Sepetu yeye ataki picha
hata moja itoke ya Diamond akiwa na Victoria Kimani kwa maana
itaendeleza kuzua maneno na kumuongezea wivu.... wakati ommy dimpoz
alipoweka picha ya yeye na Diamond wakiwa pamoja bibie wema sepetu
alifika na kuandika maneno haya na kuweka viemoji vya hasira.. huku
mashabiki wakimpoza kwa kumwambia huto ibiwa.....
Baada ya bibie wema sepetu kuweka maneno
hayo ndipo hapo Ommy Dimpoz alikuja kuondoa shari na kupeleka
mazungumzo faragha.. Ommy alijibu hivi...
HUYO VICTORIA KIMANI YUPO WAPI
Sasa wakati maandalizi ya kushoot yanaendelea, na upigaji picha ukiendelea hii ndio picha iliomuonesha Victoria kimani...
Majibu kamili yatatoka wakiamua ila
suprise imebuma kidogo..... haha... aya Diamond na Ommy watafanya show
jijini London aya tufige kwa wingi....
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni