Alizaliwa
June 16 1971
huko New York Marekani na kufariki September 13 1996 Las
Vegas Nevada Marekani baada ya kupigwa risasi zilizosababisha apelekwe University Medical Center of Southern Nevada lakini akafariki dunia siku sita baadae.
Sasa taarifa za hivi karibuni zilizotolewa na Chris Carroll ambae ni
askari polisi aliewahi kwenda kwenye eneo la tukio Tupac alipopigiwa
risasi, zinasema maneno ya mwisho yaliyotolewa na rapper huyu kwa afande
Carroll ni ‘F**k you’ na alitoa hilo tusi akiwa mikononi mwake.
Carroll
anasema alijaribu kumuuliza Tupac mara kadhaa ili amwambie anahisi ni
nani alihusika kwenye shambulio hilo la kumpiga risasi? mwishowe ndio
akatoa hilo tusi kabla ya kuchukuliwa na kupelekwa hospitali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni