Jumamosi, 31 Mei 2014

PIGO TENA BONGO MUVI: GEORGE TYSON AFARIKI DUNIA



 
George Tyson enzi za uhai wake.



 
George Tyson akimlisha keki Yvonney Chery ‘Monalisa’ wakati mtoto wao Sonia alipopata kipaimara.
NI pigo tena kwa tasnia ya Bongo Muvi, mwongozaji filamu Bongo na aliyekuwa mume wa staa wa filamu za Kibongo, Yvonny Cherry 'Monalisa', George Tyson amefariki dunia baada ya kupata ajali mbaya ya gari maeneo ya Gairo, Morogoro akitokea mkoani Dodoma. Tyson alikuwa ameambatana na watu kadhaa katika safari hiyo ambao wanadaiwa kuumia vibaya. Mwili wa marehemu Tyson pamoja na majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro. Tyson enzi za penzi lake na Monalisa walifanikiwa kupata mtoto aitwaye Sonia.
Marehemu Tyson akiwa na Monalisa (kushoto), kulia ni Tyson na mwanae Sonia.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Monalisa amemlilia Tyson kwa kuweka picha hiyo juu na kuandika maneno yafuatayo:


Monalisa akimnywesha kinywaji Tyson wakati wa kipaimara cha Sonia.
MUNGU AIPUMZISHE ROHO YA MPENDWA WETU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!
Source:GPL

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni