Jumatatu, 14 Aprili 2014

HABARI KAMILI KUHUSU Helikopta iliyoanguka IKIWA IMEMBEBA makamu wa Rais NA VIONGOZI WENGINE WAWILI


Taarifa iliyoifikia  kutoka kwa mmoja wa Waliokuwemo kwenye Helikopta hii ya jeshi inasema wakati inapaa kwenye umbali wa kama futi tano hivi kutoka uwanja wa ndege Dar es salaam,
ilizidiwa na upepo ulioirudisha nyuma na kuangukia paa kabla ya kutua chini.
Kilichofanyika ni watu waliokuwemo kutoka nje harakaharaka kisha aliekua akiiendesha kufungua tenki la mafuta na kumwaga mafuta yote alafu baada ya muda mfupi vikosi vya zimamoto vikaanza kuipiga maji helikopta hiyo ili kuepusha mlipuko.
Unaambiwa kama ingekua ni majira ya moto, helikopta hii ambayo ilikua inawapeleka kutazama maafuriko yaliyookana na mvua Dar es salaam ingeweza kuwa kwenye hatari zaidi ya kulipuka
Screen Shot 2014-04-13 at 4.37.31 PM
Ndani ya Helikopta walikuwepo watu mbalimbali akiwemo Makamu wa rais Dr. Bilal, Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Mecky Sadick.Screen Shot 2014-04-13 at 4.37.13 PM

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni