Kibongo bongo tumezoea mtu anapotaka kufunga ndoa lazima ipitishwe
michango ya kutosha ili kuweza kufanikisha sherehe, na pia mchango wako
ndio huwa kiingilio chako yaani bila kuchanga
hupati mwaliko.
Hizi ni zawadi za iPhone 5 walizopewa wageni waalikwa
Mambo yamekuwa kinyume katika harusi ya mtoto wa kike wa Rais
Goodluck Jonathan wa Nigeria aitwaye Faith, ambaye katika harusi yake
iliyofanyika jana (April 12) wageni walioalikwa wamefanyiwa surprise
kwa kupewa zawadi ya simu za iPhone 5 ‘gold plated customized’,
zilizoandikwa majina ya maharusi hao Faith na Godswill.
Juu ya mabox yaliyokuwa na zawadi ya simu hizo pameandikwa ‘Leeberry
and her Prince wish you all the best for making our day beautifull.
Thanx for coming and God Bless you’
Cha kusikitisha ni kwamba aina ya wageni wanaoweza kupata mwaliko wa
harusi kama hii ya mtoto wa mkubwa ni watu wa class flani ya watu
wanaojiweza, hivyo unaweza kukuta ni mtu ambaye tayari anayemiliki hata
iPhones mbili au tatu, so inakuwa sio big deal kivile! (Nawaza tu kwa
sauti).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni