Alhamisi, 24 Aprili 2014

DAVID MOYES KULIPWA KIAS HICHI CHA PESA BAADA YA KUTIMULIWA KUINOA MAN UNITED


Siku moja baada ya kutimuliwa kutoka kwenye kibarua cha kuif

UTAJIRI WA IRENE UWOYA WAZUA GUMZO



Inadaiwa kuwa hali ya hewa imechafuka kwa msanii nyota wa filamu za Bongo Irene Uwoya ambapo ameshindwa kutaja vyanzo vya utajiri wake wa GhaflaHivi karibuni Uwoya alikaririwa akisema kuwa

BARCA WARUHUSIWA KUUZA NA KUNUNUA WACHEZAJI BAADA YA FIFA KUTUPILIA MBALI ADHABU YAO YA AWALI.



Klabu ya Barcelona sasa inaweza kununua na kuuza wachezaji

MKE WA PETER WA P SQUARE AMETOA JIBU LA SHUTMA ZA KUSABABISHA UGOMVI WA KUNDI HILO


Wakati mashabiki wa kundi la

Magazeti ya leo tarehe 24/04/2014


AZAM KUVUNA 75M ZA UBINGWA KUTOKA VODACOM


 Meneja uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim, (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa kutangaza zawadi za washindi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambapo Azam FC ambaye ndie bingwa atanyakua Milioni 75. Timu za Yanga, Mbeya City na Simba zilizomaliza nafasi ya pili hadi ya nne zitavuna 37M, 26M na 21M zote zikiwa na nyongeza ikilinganishwa na kiasi walichozawadiwa timu zilizoshika nafasi hizo msimu uliopita wa 2012/2013.Pamoja nae katika picha, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga, (Kushoto) Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura (Kulia)Meneja Uhusiano wa Nje Vodacom Tanzania, Salum Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa kutangaza zawadi za washindi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambapo Azam FC ambaye ndie bingwa atanyakua Milioni 75. Timu za Yanga, Mbeya City na Simba zilizomaliza nafasi ya pili hadi ya nne zitavuna 37M, 26M na 21M zote zikiwa na nyongeza ikilinganishwa na kiasi walichozawadiwa timu zilizoshika nafasi hizo msimu uliopita wa 2012/2013.Wa kwanza kutoka kushoto katika picha ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga, Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura na Afisa Udhamini na Matukio  wa Vodacom, Ibrahim Kaude.
Baadhi ya Waandishi wa habari walioudhuria katika mkutano wa kutangaza zawadi kwa timu za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.Ambapo Azam FC ambaye ndie bingwa atanyakua Milioni 75. Timu za Yanga, Mbeya City na Simba zilizomaliza nafasi ya pili hadi ya nne zitavuna 37M, 26M na 21M zote zikiwa na nyongeza ikilinganishwa na kiasi walichozawadiwa timu zilizoshika nafasi hizo msimu uliopita wa 2012/2013.
*       Timu yenye nidhamu kuvuna 16M
Mdhamini Mkuu wa Ligi kuu Vodacom Tanzania Bara kampuni ya Mawasiliano  ya Vodacom imetangaza kuipatia timu ya Azam FC kitita cha Sh 75 kama zawadi ya fedha taslimu baada ya kuibuka bingwa wa ligi msimu wa 2013/2014.
Mwaka jana Bingwa wa Ligi Kuu Vodacom ambapo ilikuwa timu ya Yanga alizawadiwa kitita cha Sh 70 Milioni.
Zawadi hiyo imetangazwa leo jijini Dar es salaam na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania - TFF.
"Tunayofuraha kubwa leo kuzitangaza zawadi za fedha taslimu kwa bingwa wetu mpya na wengine walioshika nafasi ya pili hadi ya nne, tunajisikia furaha kutimiza yale yaliyo kwenye mkataba wetu wa udhamini wa ligi."Alisema Mwalim
Timu za Yanga, Mbeya City na Simba zilizomaliza nafasi ya pili hadi ya nne zitavuna 37M, 26M na 21M zote zikiwa na nyongeza ikilinganishwa na kiasi walichozawadiwa timu zilizoshika nafasi hizo msimu uliopita wa 2012/2013.
Mwalim amesema Vodacom itaendelea kufanya kila lililo ndani ya uwezo wake kuboresha ligi ikiwemo zawadi ili kuongeza kasi ya ushindani miongoni mwa timu shiriki za ligi.
Amesema Vodacom itatumia zaidi ya Sh 210 kwa ajili ya zawadi za fedha kwa timu zilizoshika nafasi nne za juu pamoja na timu nyengine zilizoonesha umahiri katika maeno mengine ikiwemo timu yenye nidhamu itakayovuna 16M.
"Tunatambua kuwa bado zipo changamoto za hapa na pale ikiwemo eneo la zawadi, na matazamio na matarajio ya watanzania hususan wapenda soka bado ni makubwa lakini angalau sasa tumefika mahala tunapoweza kujivunia hadhi na mahala ligi ilipo wakati safari ya mafanikio zaidi ikiendelea."
Wengine watakaovuna fedha kutoka Vodacom ni pamoja mchezaji bora (5.2M), mfungaji bora (5.2M), mlinda mlango bora 5.2M), mwamuzi bora na mwalimu bora 7.8 kila mmoja.
"Shabaha yetu ni kutafuta namna bora ya ligi yetu kuwa bora zaidi ya hapa tulipofika ili kuvutia wawekezaji zaidi, ni kwa njia hiyo tutafikia mafanikio makubwa zaidi ya kuwa na ligi kubwa, yenye ushindani na mvuto wa juu zaidi ndani na nje ya nchi..'Alisema Mwalim
Mwalim ametumia nafasi hiyo kuendelea kuzipongeza timu zote 14 zilizoshiriki ligi huku akiutaja msimu wa 2013/2014 kuwa ulikuwa bora zaidi ya msimu uliopita wa 2012/2013.
Mwisho





 Meneja uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim, akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa kutangaza zawadi za washindi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambapo Azam FC ambaye ndie bingwa atanyakua Milioni 75. Pamoja nae katika picha, wa kwanza kutoka kulia niAfisa Habari wa TFF, Boniface Wambura  na Afisa Matukio na Udhamini wa Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude

Jumatatu, 14 Aprili 2014

MAGAZETI YA UDAKU LEO

BREAKING NEWS MZEE GURUMO AFARIKI DUNIA

Screen Shot 2014-04-13 at 5.10.14 PM 


Ni mzee wa siku nyingi sana kwenye muziki Tanzania ambae aliwahi kuingia kwenye vichwa vya habari mara nyingi hasa kutokana na kuugua kwake kuliko mfanya aache hata muziki aliokua anaufanya.
Taarifa zilizothibitishwa na hospitali ya Taifa Muhimbili
zimesema Mzee huyu amefariki dunia akiwa hospitalini hapo leo April 13 2014 saa nane mchana baada ya kuletwa jana asubuhi na kulazwa kwenye wodi namba 6 ya Mwaisela kutokana na kuzidiwa. Tayari mwili wake umepelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti ambapo taarifa zaidi kuhusu chanzo cha kifo na taratibu za mazishi blogu ya wananchi itaendelea kuzitoa

HABARI KAMILI KUHUSU Helikopta iliyoanguka IKIWA IMEMBEBA makamu wa Rais NA VIONGOZI WENGINE WAWILI


Taarifa iliyoifikia  kutoka kwa mmoja wa Waliokuwemo kwenye Helikopta hii ya jeshi inasema wakati inapaa kwenye umbali wa kama futi tano hivi kutoka uwanja wa ndege Dar es salaam,
ilizidiwa na upepo ulioirudisha nyuma na kuangukia paa kabla ya kutua chini.
Kilichofanyika ni watu waliokuwemo kutoka nje harakaharaka kisha aliekua akiiendesha kufungua tenki la mafuta na kumwaga mafuta yote alafu baada ya muda mfupi vikosi vya zimamoto vikaanza kuipiga maji helikopta hiyo ili kuepusha mlipuko.
Unaambiwa kama ingekua ni majira ya moto, helikopta hii ambayo ilikua inawapeleka kutazama maafuriko yaliyookana na mvua Dar es salaam ingeweza kuwa kwenye hatari zaidi ya kulipuka
Screen Shot 2014-04-13 at 4.37.31 PM
Ndani ya Helikopta walikuwepo watu mbalimbali akiwemo Makamu wa rais Dr. Bilal, Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Mecky Sadick.Screen Shot 2014-04-13 at 4.37.13 PM

Matokeo ya Liverpool vs Man City April 13 umeyapata? yako hapa

Mechi ilivyoanza tu wachambuzi wa soka waliona kama leo Liverpool itampiga mtu nyingi sana ila mwishoni ndio matokeo yakawa hivi… Liverpool 3 – 2 Manchester City.Screen Shot 2014-04-13 at 6.55.47 PM

Jumapili, 13 Aprili 2014

UKISTAAJABU YA MUSSA UTAYAONA YA FILAUNI!! CHEKI HIZI PICS



Baada ya kuwa tunajiuliza inakuwaje watu wazima na wanaojielewa wanapiga picha za hivi na kutopata majibu, tumepigwa na butwaa baada ya hili kutokea. Huyu binti ni mtoto wa Rais wa Cape Verde. Pamoja na kuwa na pesa, na kila kitu katika maisha lakini kaamua kufanya huu ujinga