Alhamisi, 24 Aprili 2014

DAVID MOYES KULIPWA KIAS HICHI CHA PESA BAADA YA KUTIMULIWA KUINOA MAN UNITED


Siku moja baada ya kutimuliwa kutoka kwenye kibarua cha kuif

UTAJIRI WA IRENE UWOYA WAZUA GUMZO



Inadaiwa kuwa hali ya hewa imechafuka kwa msanii nyota wa filamu za Bongo Irene Uwoya ambapo ameshindwa kutaja vyanzo vya utajiri wake wa GhaflaHivi karibuni Uwoya alikaririwa akisema kuwa

BARCA WARUHUSIWA KUUZA NA KUNUNUA WACHEZAJI BAADA YA FIFA KUTUPILIA MBALI ADHABU YAO YA AWALI.



Klabu ya Barcelona sasa inaweza kununua na kuuza wachezaji

MKE WA PETER WA P SQUARE AMETOA JIBU LA SHUTMA ZA KUSABABISHA UGOMVI WA KUNDI HILO


Wakati mashabiki wa kundi la

Magazeti ya leo tarehe 24/04/2014


AZAM KUVUNA 75M ZA UBINGWA KUTOKA VODACOM


 Meneja uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim, (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa kutangaza zawadi za washindi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambapo Azam FC ambaye ndie bingwa atanyakua Milioni 75. Timu za Yanga, Mbeya City na Simba zilizomaliza nafasi ya pili hadi ya nne zitavuna 37M, 26M na 21M zote zikiwa na nyongeza ikilinganishwa na kiasi walichozawadiwa timu zilizoshika nafasi hizo msimu uliopita wa 2012/2013.Pamoja nae katika picha, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga, (Kushoto) Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura (Kulia)Meneja Uhusiano wa Nje Vodacom Tanzania, Salum Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa kutangaza zawadi za washindi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambapo Azam FC ambaye ndie bingwa atanyakua Milioni 75. Timu za Yanga, Mbeya City na Simba zilizomaliza nafasi ya pili hadi ya nne zitavuna 37M, 26M na 21M zote zikiwa na nyongeza ikilinganishwa na kiasi walichozawadiwa timu zilizoshika nafasi hizo msimu uliopita wa 2012/2013.Wa kwanza kutoka kushoto katika picha ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga, Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura na Afisa Udhamini na Matukio  wa Vodacom, Ibrahim Kaude.
Baadhi ya Waandishi wa habari walioudhuria katika mkutano wa kutangaza zawadi kwa timu za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.Ambapo Azam FC ambaye ndie bingwa atanyakua Milioni 75. Timu za Yanga, Mbeya City na Simba zilizomaliza nafasi ya pili hadi ya nne zitavuna 37M, 26M na 21M zote zikiwa na nyongeza ikilinganishwa na kiasi walichozawadiwa timu zilizoshika nafasi hizo msimu uliopita wa 2012/2013.
*       Timu yenye nidhamu kuvuna 16M
Mdhamini Mkuu wa Ligi kuu Vodacom Tanzania Bara kampuni ya Mawasiliano  ya Vodacom imetangaza kuipatia timu ya Azam FC kitita cha Sh 75 kama zawadi ya fedha taslimu baada ya kuibuka bingwa wa ligi msimu wa 2013/2014.
Mwaka jana Bingwa wa Ligi Kuu Vodacom ambapo ilikuwa timu ya Yanga alizawadiwa kitita cha Sh 70 Milioni.
Zawadi hiyo imetangazwa leo jijini Dar es salaam na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania - TFF.
"Tunayofuraha kubwa leo kuzitangaza zawadi za fedha taslimu kwa bingwa wetu mpya na wengine walioshika nafasi ya pili hadi ya nne, tunajisikia furaha kutimiza yale yaliyo kwenye mkataba wetu wa udhamini wa ligi."Alisema Mwalim
Timu za Yanga, Mbeya City na Simba zilizomaliza nafasi ya pili hadi ya nne zitavuna 37M, 26M na 21M zote zikiwa na nyongeza ikilinganishwa na kiasi walichozawadiwa timu zilizoshika nafasi hizo msimu uliopita wa 2012/2013.
Mwalim amesema Vodacom itaendelea kufanya kila lililo ndani ya uwezo wake kuboresha ligi ikiwemo zawadi ili kuongeza kasi ya ushindani miongoni mwa timu shiriki za ligi.
Amesema Vodacom itatumia zaidi ya Sh 210 kwa ajili ya zawadi za fedha kwa timu zilizoshika nafasi nne za juu pamoja na timu nyengine zilizoonesha umahiri katika maeno mengine ikiwemo timu yenye nidhamu itakayovuna 16M.
"Tunatambua kuwa bado zipo changamoto za hapa na pale ikiwemo eneo la zawadi, na matazamio na matarajio ya watanzania hususan wapenda soka bado ni makubwa lakini angalau sasa tumefika mahala tunapoweza kujivunia hadhi na mahala ligi ilipo wakati safari ya mafanikio zaidi ikiendelea."
Wengine watakaovuna fedha kutoka Vodacom ni pamoja mchezaji bora (5.2M), mfungaji bora (5.2M), mlinda mlango bora 5.2M), mwamuzi bora na mwalimu bora 7.8 kila mmoja.
"Shabaha yetu ni kutafuta namna bora ya ligi yetu kuwa bora zaidi ya hapa tulipofika ili kuvutia wawekezaji zaidi, ni kwa njia hiyo tutafikia mafanikio makubwa zaidi ya kuwa na ligi kubwa, yenye ushindani na mvuto wa juu zaidi ndani na nje ya nchi..'Alisema Mwalim
Mwalim ametumia nafasi hiyo kuendelea kuzipongeza timu zote 14 zilizoshiriki ligi huku akiutaja msimu wa 2013/2014 kuwa ulikuwa bora zaidi ya msimu uliopita wa 2012/2013.
Mwisho





 Meneja uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim, akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa kutangaza zawadi za washindi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambapo Azam FC ambaye ndie bingwa atanyakua Milioni 75. Pamoja nae katika picha, wa kwanza kutoka kulia niAfisa Habari wa TFF, Boniface Wambura  na Afisa Matukio na Udhamini wa Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude