Jumatano, 2 Julai 2014

ALI KIBA NA LADY JAYDEE KUPANDA JUKWAA MOJA NA NICKI MINAJ SEPT, AFRIKA KUSINI

Ali Kiba na Lady Jaydee wanatarajiwa kupanda jukwaa moja na rapper Nicki Minaj, Macklemore and Ryan Lewis, J Cole na Kid Ink kwenye tamasha kubwa zaidi kuwahi kutokea barani Afrika, la Tribeone Dinokeng’ litakalofanyika Tshwane, nchini Afrika Kusini mwezi September mwaka huu.



Wasanii wengine wa Afrika watakaotumbuiza ni pamoja na Jaguar, Redsan, Nameless na Xtatic wa Kenya, Wizkid wa Nigeria, Fally Ipupa wa Congo, Maurice Kirya, Keko, Naava Grey wa Uganda pamoja na rappers wa Afrika Kusini, Khuli Chana na AKA.


Tamasha la ‘TribeOne Dinokeng’ limeandaliwa na ROCKSTAR4000 na Sony Music Entertainment na litafanyika 26-28 September.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni