Mkazi wa Kitangiri jijini Mwanza, Biera Edwin (22) amelazwa katika
Hospitali ya Rufaa ya jiji Sekou Toure akipatiwa matibabu baada ya
kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake kwa tuhuma za kuwa na
mahusiano ya kimapenzi na mume wa mtu.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola hakupatikana kuzungumzia
tukio hilo, lakini Biera mwenyewe alisema kabla ya kufanyiwa kitendo
hicho mama ambaye ni jirani yao
alimtuma mtoto wake amwite nyumbani kwao, alipokwenda mama huyo alianza kumshambulia.
Alisema
alimshambulia akishirikiana na marafiki zake na kumjeruhi vibaya kwa
nyaya za umeme, kumwingizia chupa kwenye sehemu zake za siri na baadaye
kuchoma nguo zake.
Binti huyu kwa sasa amelazwa katika wadi ya
majeruhi kwenye Hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure akipatiwa
matibabu na alisema baada ya kufanyiwa ukatili huo pia waliteketeza nguo
zake kwa moto.
Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza,Valentino mlowola
Naye
dada wa majeruhi, Nice Cosmas anaeleza kuwa akiwa nyumbani kwao, mama
huyo wa jirani alituma watoto wake ambao walieleza kuwa wakamchukue mtu
wao.
Alisema walipokwenda hapo jirani alimkuta ndugu yake akiwa hana nguo huku akiwa amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake.
Alisema
walilazimika kurudi nyumbani kumchukulia nguo za kumvisha na kisha
kutoa taarifa kwa mamlaka husika kabla ya kumpeleka hospitali kwa
matibabu.
Baadhi ya viongozi wa mtaa wa Kitangiri A
walisikitishwa na kitendo hicho na kuomba vyombo vya sheria kuwachukulia
hatua kali wahusika.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kitangiri A, Issa Salum alisema wanataka haki itendeke kwani kitendo hicho ni nusu ya mauaji.
Naye
Mjumbe wa Serikali za Mitaa, Mariam Yusuf alisema mama huyo wa jirani
alipaswa kutoa taarifa kwa mabalozi ama kwa wazazi wa binti huyo kama
alikuwa na uhakika na madai yake kabla ya kuchukua ukatili dhidi ya
binti huyo